Koitaleel Samoei University College

Koitaleel Samoei University College

SIKU YA KISWAHILI DUNIANI

_By Carias Osano

Chuo kikuu Cha koitaleel kinaungana na ulimwengu katika kusherekea siku ya kiswahili DUNIANI.

Waswahili husema masukuzi ya leo ndio msitu wa kesho tupalilie na kukikuza Kiswahili leo ili kije kiwafae wengine. Tuimarishe semi zetu, acha zinuke shombo, lakini shombo ya Kiswahili.

Acha tule kama Waswahili, tuvae kama Waswahili, tutembee kama Waswahili, .kwani ni nani asiyejua kuwa pofu haachi mkongojowe?

Heko kwa wale wanaokikuza kiswahili lugha yenye ukwasi mkubwa wa wazungumzaji barani Afrika. Tuzidi kuwa pamoja katika kupuliza Kiswahili dawa ili kisije kikavamiwa na vimelea kama vile sheng’, kukipaka mafuta ili kuzidi kuwa safi na kukipaka manukato ili kuzidi kunukia na kuvutia.

Acha kiswahili kitukuzwe ili tuondoe falsafa inayoaminika na baadhi ya ndugu wa lugha ya wazungu kuwa bora zaidi. Mtazamo wetu kama Waswahili uwe juu sana. Tufaane kufaana katika kukuza hii lugha.

Japo mashambulizi yamechacha, tutie bidii za mchawa wajengao vingulima kwa mate yao kama si sondomti watoboao gogo kwa vinywa vyao bila msimamizi.

Sina mengi ila hisani hulipwa na hisani. Hongereni enyi mnaozidi kukiimarisha Kiswahili . Nawavika koja, nawapa takrima na Qudusi azidi kuwa nanyi miaka na dahari .

Asilani tusilegee kukiinua Kiswahili juu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top